Mamlaka ya Maji Safi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASA) inatarajia kununua magari kwa ajili ya kubebea majitaka kwenye nyumba za watu ili kurahisisha huduma hiyo kutokana na sekta binafsi kuwatoza gharama kubwa wananchi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja, amesema hatua hiyo inalenga DAWASA kujitosa katika shughuli hiyo ili kuwasaidia wananchi ambapo wao watakuwa na bei ya kawaida pindi watakapoanza kutoa huduma hiyo, ikilinganishwa na sekta binafsi.
“Malori yetu yatafanya kazi hiyo kwani mtandao wa majitaka ni mdogo, private sector zinatoza gharama kubwa hivyo inachangia wananchi kutumia mwanya wa mvua kufungulia majitaka,”amesema.
POLISI WALIVYOWATIA MBARONI WAVUVI 43 ‘WAMELIPA FAINI MIL.4’