Kanda ya kaskazini ya tour ya Ali Kiba imekamilishwa na Namanga sehemu ambayo ni mpaka wa Tanzania na Kenya ambapo asilimia kubwa ya wakazi wa huku ni Watanzania ambao pia huwa wanapata ugeni wa wakazi kutoka Kenya yanapotokea matamasha makubwa.
Show iliyofanyika Namanga ilipata heshima ya kuwa na wakazi wa Nairobi Kenya ambao waliamua kuvuka mpaka na kuja kushuhudia show ya Ali Kiba ambapo Ali alipoongea na millardayo.com amesema tour hii bado inaendelea na itaenda nchi kadhaa ikiwemo Rwanda, Burundi, Congo, Kenya na Uganda.
Hizi ni badhi ya picha wakati Ali Kiba, Abdul kiba na Recho waliposimama mbele ya mashabiki zao Namanga.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook