Staa maarufu kutokea Marekani Alicia Keys ambaye alitamba na ngoma zake kali miaka kadhaa iliyopita ikiwemo Girl On Fire, No One, Fallin na nyingine nyingi ameonyesha kukubali vipaji vinavyoonyeshwa na watoto wadogo na hii ni baada ya kupost video clip ya mtoto kutokea Kenya.
Kutokana na staa huyo kupost video clip ya msichana mdogo akiimba wimbo wake wa “Girl on fire” comments zimekuwa nyingi kutoka kwa mashabiki na kumtaka amsaidie mtoto huyo ili atimize ndoto zake za uimbaji.
Alicia Keys aliandika “Angalia nafsi hii yenye kushangaza, Ng’aa”
Dj Khaled, P Diddy, Snoopy Dog, Chris Brown na mastaa wengine wengi wamewahi pia kuonyesha kukubali na kuthamani vipaji vinavyoonyeshwa na watu kutokea bara la Afrika kupitia kurasa zao za instagram.
King Majuto “Zipo Kampuni nimefanya kazi, mikataba ninayo wamekimbia na hela zangu”