Fahamu kwamba mwaka 1993 msanii wa Rap kutokea Marekani Marehemu Tupac alipata barua kutoka kwa wazazi wa kijana mwenye umri wa miaka 11 aliyekuwa akikaribia kufa aliyetambulika kwa jina la Joshua Tores na kusema kuwa alitamani kukutana na rappa huyo.
Baada ya marehemu Tupac kupata barua hiyo aliamua kusafiri na kuelekea jijini Maryland nchini Marekani October 14,1993 ili kutimiza ndoto ya kijana Joshua na alipofika aliamua kumpeleka katika uwanja wa basketball na walifanikiwa kuongea vitu vingi kwa nusu saa.
Baada ya saa mbili kupita taarifa za kifo cha Joshua zilimfikia marehemu Tupac na alitaka kufanya kitu kwaajili ya kumuenzi kijana huyo ambaye alimpenda na hivyo kuamua kubadilisha jina la kampuni yake ya uchapishaji kutoka “Ghetto Gospel Music” mpaka “Joshua’s Dream”
Marehemu Tupac alifariki September 13,1996 na aliacha pengo kubwa katika muziki wa rap duniani na pia aliacha historia kubwa kutokana na ukarimu aliokuwa akiuonyesha kwa vijana wadogo wenye ndoto kubwa katika game ya muziki.
Gigy Money alilimiss buku la Mo J “tunataka kuzaa mtoto wa kiume”