Baada ya Beyonce na Jay Z kukusanya mabilioni ya pesa katika ziara yao ya On The Run II iliyofanyika nchi mbalimbali ikiwa bado inaendelea, wameamua kutumia fedha hizo kwa ajili ya watoto wa shule watakaojiunga na chuo kikuu mwaka huu.
Inaripotiwa kuwa wawili hao wametoa kiasi cha dola Millioni 1 za Kimarekani sawa na Billioni 2 za Kitanzania kwaajili ya ufadhili wa wanafunzi hao wenye uhitaji wakati wakijiandaa kuanza elimu ya chuo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na waandishi wa habari, ufadhili huo utahusisha fedha zaidi ya Tsh Millioni 200 kwa kila mwanafunzi ambazo zitawekwa kwenye akaunti ya kila mmoja kwa lengo la kuwasaidia kimasomo na mahitaji mengine kwa mwaka mzima.
Wanafunzi hao watachujwa kupitia mtandao wa The Boys and Girls Club na watatoka kwenye miji ambayo ziara hiyo imefanyika ikiwemo Atlanta, Orlando, Miami, Huoston, Los Angeles na Santa Clara
RC Kagera atoa tamko “Hatujamtuma Mwalimu kuchapa, acha sheria ifanye kazi”