Leo November 12,2018 muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ amekamilisha kutumikia kifungo chake cha nje na sasa yupo huru kujihusisha na maisha yake ya kawaida ambapo May 14,2018 Mahakama Kuu ya Tanzania ilimuachia huru ili akatumikie kifungo cha nje.
Kwa mujibu wa post ya instagram ya Dr Cheni ambaye ni mtu wa karibu na Elizabeth Michael ameonyesha furaha aliyonayo na kuwashukuru wale wote waliokuwa karibu na lulu kipindi chote na kumsisitiza Majizzo afanye haraka kuhusu mchakato wa ndoa.
“Sina la kusema @elizabethmichaelofficial zaid ya kumshukuru Mungu na kumwambia Mungu Asantee Kwa hili jambo kuisha salama Unajuwa jinsi gani lilituumiza kichwa ila Watanzania wenye mapenzi mema na wewe walikuombea kila Saa kila dakika. Sasa wakati mwengine unaenda kuanza Maisha upya na mapya Karibu uraian tuje kupambana wote na imani”
“Mungu anaenda kukutendea Miujiza mikubwa katika Maisha yako Mwanzo tuliona Ni Muda Kama hauwendi kumbe kila kitu ukimwachia Mungu siku zinakimbia kuliko kweli Mungu Ni mwema natumai @elizabethmichaelofficialumemuona Mungu ajakuacha nikuombe Nawe usimwache MUNGU”
“Nichukuwe Nafasi ya kuwashukuru wote mliokuwa nasi kwenye kipindi muhimu na kigumu najuwa mlimuombea Kwa kila mtu na imani yake basi msiache kumuombea niwashukuru hata wale ambao hawakuweza kuwa Karibu nasi Ila naiman mlituombea Muda mwingi nikushukuru sana tena sana baba mkwe Mtarajiwa @majizzo we mtu unaroho ya kipekee sana”
“Mtu akikutazama Kwa nje anaweza asipate jibu Ila moyo wako Ni wakipekee sana nimejifunza kitu kutoka kwako.na nahisi ninamaneno mengi sana Ila la Mwisho kwako @majizzo nikukumbushe tu au nisisitize ile Pete isiwe Mwisho wa safari yenu naomba taratibu za mwisho ziendelee haraka japo najuwa kwako hilo halina tatizo ili Ndoa ipite sasa dogo sasa yupo Huru”
Amber Rutty alivyofikishwa Mahakamani Kisutu baada ya kukosa dhamana