Daktari wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Hamis Nikuli amesema changamoto ya uzalishaji wa samaki katika maji ya asili umekuwa ukipungua, huku mahitaji yakiwa ni makubwa kutokana na idadi ya watu kuongezeka ambapo watu wanakula Kilo 8 kwa mwaka badala ya Kilo 17.
Dk.Nikuli amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa ili kufikia kiwango hicho inahitajika kufuga zaidi samaki ili kufikia mahitaji hayo kwa kutumia teknolojia ambayo inazalisha samaki wengi kwa muda mfupi.
Amesema katika suala hilo la ufugaji wa samaki kuna mambo ya kuzingatia ikiwemo kutoweka samaki wengi katika eneo moja kwani linaweza kusababisha magonjwa ili wafugaji wasiweze kupata hasara na afya ya walaji inaimarika.