Msanii maarufu kutokea +254 Kenya Prezzo amethibitisha kumaliza beef lake na msanii mwenzake ambaye kwa sasa ni Mbunge katika jimbo la Starehe Charles Njagua maarufu kama “Jaguar “ na kulithibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram.
“Kama wengi mnavojua mimi na ndugu yangu @jaguarkenya tulkuwa na friction miaka nenda, miaka rudi ila Mungu alitupatanisha tukaamua kusahau yalio pita na focus kwa ya lio mbele. Iam glad we burried the hatchet now lets put in work my brother Bless up #Rapcellency“
Beef kati ya Prezzo na Jaguar linafahamika kuwa ni la muda mrefu takribani zaidi ya miaka 3 na mwaka huu wa 2018 umekuwa ni wa baraka kwao na kumaliza tofauti zao na huenda kutokana na kupatana kwao tukapata collabo kali kutoka kwao.
ALIKIBA ALIVYOMVALISHA PETE MKEWE AMINA -ViaAzam TV