Top Stories

Baraza la Habari latoa tamko baada ya Wanaharakati wa CPJ kuachiwa huru

on

Baraza la Habari Tanzania (MCT), Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) na Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC) umelaani vikali kitendo cha kukamatwa kwa Maafisa wa Kamati ya Ulinzi wa Waandishi, Angela Quintal(raia wa Afrika Kusini) na Muthoki Mumo(raia wa Kenya).

Kaimu Katibu Mtendaji wa MCT, Pili Mtambalike amewaambia waandishi wa habari kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vifanye kazi zake kwa weledi na kwa mujibu wa sheria za nchi na mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imeridhia ili kudumisha amani, upendo na mshikamano.

“Vyombo hivi tunaviasa kwa namna yoyote ile visifanye kazi zake kwa hisia bali vifuate taratibu za nchi za kisheria ili visiwe chanzo cha kuvurugika kwa amani na uhusiano na mataifa mengine na kupeleka Watanzania na jumuiya ya kimataifa kutokuwa na imani navyo,”amesema Mtambalike

Indaiwa kuwa Wanaharakati hao, walikamatwa na watu watatu ambapo mmoja alijitambulisha kuwa ni Afisa wa Idara ya Uhamiaji November 7, 2018 saa 4:30 usiku katika Hoteli ya Southern Sun iliyopo jijini Dar es Salaam.

Inaelezwa kuwa tayari wanaharakati hao wameshaachiwa huru tangu November 8, 2018 ambapo wamerudishiwa hati zao za kusafiria.

FULL VIDEO: Tabasamu la Miss Tanzania akikwea Pipa kuelekea China

Soma na hizi

Tupia Comments