Arsenal na Chelsea tayari wako jijini Baku kwa ajili ya fainali ya Europa usiku wa leo, London ni jiji la pili tu kuwahi kufikisha timu mbili katika fainali ya mashindano ya vilabu Ulaya, Madrid ndio lilikuwa jiji la kwanza na wamefanya hivyo mara mbili, 2014 na 2016 ambapo Real na Atletico walifika fainali pamoja, lakini mwaka huu ni zamu ya London.
Kocha wa Arsenal Unai Emery, ambaye amewahi kushinda Kombe hilo mara tatu mfululizo akiwa na Sevilla ana changamoto kubwa kwenye kupanga kikosi chake katika nafasi ya mlinda mlango. Pert Cech, ambaye amekuwa akidaka kwenye mechi za Europa, anahusishwa kujiunga na Chelsea kwenye nafasi ya Mkurugenzi wa Ufundi.
Baadhi ya wachambuzi wanashauri Emery kutokana na hali ilivyo amuanzishe mlinda mlango chaguo la kwanza Bernd Leno nafasi ya kuanza kwenye mchezo huo jijini Baku, Emery atamkosa kiungo mshambuliaji Henrikh Mkhitaryan, ambaye hakusafiri na timu inayokwenda kucheza katika dimba la Olympic Stadium kwenye mji mkuu wa Azerbaijan.
Mkhitaryan ambaye ni raia wa Armenia – nchi ambayo haina mahusiano mazuri ya kidiplomasia na Azerbaijan. Nchi hizo pia zina ugomvi ambao unaendelea hadi sasa wakigombania ukanda ambao upo ndani ya mipaka ya Azerbaijan.
Naye kocha wa Chelsea, Maurizio Sarri atawakosa baadhi ya wachezaji wake. Chelsea ambao walicheza mechi ya hisani nchini Marekani baada ya msimu wa ligi kuisha na kiungo Ruben Loftus-Cheek kuuma huku wakishinda kwa magoli 3-0 dhidi ya New England Revolution, game itaoneshwa ST World Football.
EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega