Wakati Mawakili 909 nchini Tanzania wakihitimu leo December 14, 2018 Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma amesema ufasaha wa lugha ya Kiingereza kwa mawakili bado ni changamoto, hivyo kulingana na karne ya sasa hawana budi kujiendeleza kielimu.
Katika shughuli hiyo ambayo imehudhuriwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk Adelardus Kalangi, Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Fatma Karume, mawakili na majaji wastaafu, Profesa Juma amesema mawakili hao wamepita safari ndefu ya masomo ila ufanisi katika kujieleza kwa lugha ya Kiingereza upo chini.
Amesema ili kuhimili ushindani, kufahamu lugha ya Kiingereza kwa wanataaluma wa kada hiyo ni jambo lisilokwepeka na kuwataka mawakili kuendelea kujinoa.
“Niseme kuwa ufasaha katika kujieleza kwa lugha ya Kiingereza ni changamoto inayotakiwa kufanyiwa kazi au uongo? “