Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imezungumzia jinsi inavyodhibiti biashara za vipodozi kwa kufanya tathimini, ambapo pia imetaja mikoa ambayo watu wake wanaongoza kujichubua (Mikorogo).
Mkurugenzi wa TFDA, Adam Mitangu amewaambua waandishi wa habari kuwa udhibiti wa vipodozi upo wa aina nyingi ikiwemo kufanya tathimini ya uwepo wa viambata vya sumu ambapo wanatumia maabara pamoja na kufanya ukaguzi katika vituo vya forodha.
“Kwa uzoefu wetu tumeiona mikoa inayoongoza kwa watu wake kujichubua hasa kutokana na baridi ikiwemo Mbeya, Njombe na Tabora,”amesema.