Hii ni ya kuifahamu kutokea Nigeria inayomuhusu staa wa muziki Kiss Daniel ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake ya “Yeba” kubadilisha jina lake na kujiita Kizz Daniel ikiwa wengi walimzoea kwa jina lake la kisanii la Kiss Daniel
Staa huyo alifikishwa mahakamani mwanzoni wa mwezi January na music label ya G Worldwide aliyokuwa akifanya nayo kazi kwa kipindi kirefu na kudai kuwa alivunja masharti yaliyokuwa kwenye mkataba huo kwa kuamua kuanzisha label yake mwenyewe ya Fly Boy Inc
Kutokana na uvunjaji wa masharti ya mkataba kampuni hiyo ya G WorldWide iliamua kumpiga marufuku staa huyo kutumia jina la Kiss Daniel na ndio sababu ya kubadilisha jina na kutumia Kizz Daniel.
EXCLUSIVE: Nyoshi kafunguka kutumia mkorogo, ametaja mastaa wanaotumia