Leo July 10, 2017 Rais Magufuli amekabidhiwa nyumba za wahudumu wa afya na Mkapa Foundation katika sherehe iliyofanyika kijiji cha Mkungo, Wilaya ya Chato, Geita.
Haya hapa mambo makubwa 12 Rais Magufuli ameyazungumza wakati wa sherehe ya kukabidhiwa nyumba hizo ambapo ameipongeza pia Mkapa Foundation akisema anazipenda Taasisi zinazofanya kazi ya kuonekana na sio zinazoongea ongea.
'Hata mimi yupo mtoto wa mdogo wangu amezalia nyumbani, mtoto anamuita John wa pili anamuita Samia lakini hakubakwa'- Rais @MagufuliJP
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
'taasisi za kila siku kwenye majukwaa mzinyime fedha nataka taasisi zinazofanya kazi inayoonekana sio za kuongea ongea tu'- Rais @MagufuliJP
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
Tunafanya ukaguzi nchi nzima kuwajua waliotumia vibaya fedha za pembejeo ambazo ni zaidi ya hhilingi bilioni 1.5' – Rais @MagufuliJP #CHATO
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
'Mimi nazipenda sana taasisi zinazofanya kazi kama hii ya Mkapa Foundation sio zinazotaka watoto wazae wakiwa shule' – Rais @MagufuliJP
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
'Nilipoletewa miswada ya madini iliyopitishwa Bungeni niliisaini siku hiyo hiyo na hivi karibuni tutaanza mazungumzo'- Rais @Magufuli
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
'Naibu Waziri Kalemani yupo na nimeagiza kuanzia sasa hakuna kutoa leseni yoyote ya madini, ukitoa na wewe upotelee huko huko' @MagufuliJP
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
'Mzee Mkapa umejenga nyumba nyingi ungeweza kuzitumia kufanya biashara lakini umezigawa bure, unastahili pongezi'- Rais @MagufuliJP #CHATO
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
'Tumefanya ukaguzi wa mikoa 11 madeni yalikuwa bilioni 50 lakini baada ya ukaguzi tumegundua madeni halali ni bilioni 8' – Rais @MagufuliJP
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
'Najua Geita ni mkoa wa mwisho kujengwa kwa nyumba hizi, lakini watapindisha maneno na kusema zinajengwa kwa Magufuli' – Rais @MagufuliJP
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
'Namshukuru sana Waziri wa Afya anafanya kazi vizuri na anafuata maagizo ninayompa kama suala la bei ya madawa' – Rais @MagufuliJP #CHATO
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
'Najua mzee Mkapa hupendi sifa ila naomba nishukuru kwa kuniamini na kuniteua kwenye nafasi mbalimbali Serikalini' – Rais @MagufuliJP #CHATO
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
'Ninamuomba sana Mwenyenzi Mungu asinifanye nikawa na kiburi na kusahau nilikotoka' – Rais @MagufuliJP #Chato
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
“Sasa hivi tumeweka sheria mpaka majipu yanajitumbua yenyewe” – JPM!!!