Marehemu Ivan Semwanga maarufu kama Ivan Don amefikisha mwaka mmoja kamili tokea afariki dunia May 25,2017 katika hospitali ya Steve Biko Academic iliyopo Pretoria Afrika Kusini na kuzikwa kwao Uganda.
Kupitia ukurasa wa instagram wa Zari ambaye alikuwa mzazi mwenzake na marehemu Ivan Don ameandika maneno ya kumuenzi na kuzidi kumuombea popote pale alipo ikiwa watoto wake watatu bado wanamkumbuka baba yao.
“Mwaka mmoja umepita tokea uitwe mbele ya haki, Mungu amekuchukua nyumbani kwa mapenzi yake lakini mioyoni mwetu utaishi milele, ninachokifahamu ni kuwa hatupotezi wapendwa wetu kwenye kifo bali wanaendelea kushiriki katika maisha yetu ya kila siku kupitia maamuzi yetu tunayofikiria.”
“Mimi na wanao tunashukuru kujua kuwa maisha yetu yamekuwa katika mapenzi yako ,wale ambao tunawapenda huwa hawaondoki bali wanatembea pembeni yetu kila siku, hatuwaoni wala kuawaskia lakini wapo karibu yetu.
“Bado tunakupenda na tutazidi kukumbuka najua unatabasamu huko uliko katika mawingu ya neema ya Mungu Pumzika kwa Amani Don”
Dulla Makabila kazungumza baada ya skendo kubaka “Nilitembea na mwanafunzi”