July 27, 2017 Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Sita wa mwaka wa Wahariri na Waandishi Waandamizi ulioandaliwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa ‘TANAPA’ lengo likiwa ni kukuza na kuimarisha utalii wa ndani wa nchi.
Moja ya mambo aliyoyagusia katika hotuba yake kwa Wanahabari ni kuwa Tanzania ingali inakabiliwa na tatizo la ujangili ambao ingawa limeonekana kupungua kutokana na mchango wa Wanahabari kuripoti matukio kadhaa ikiwemo adhabu zinazotolewa kwa majangili waliokamatwa.
>>>”Ujangili bado upo lakini nataka niseme wazi, Majangili tumepambana nao kweli kweli na ninyi mmetusaidia kueneza habari za Majangili kukamatwa na kufungwa miaka mingi kitu ambacho kimefanya watu wengi waanze kuogopa kujihusisha na biashara hii.
“Hii inaonesha kabisa ni namna gani mmefanya kazi kubwa ya kuhabarisha madhara ya watu kushiriki kwenye biashara hii ya ujangili kwa sababu huko nyuma watu walikuwa wanaona kawaida kuona hata Tembo wakiuawa ovyo lakini imekuwa tofauti sana kwa sasa.” – Waziri Maghembe.
ULIPITWA? Kauli ya Naibu Spika Dr. Tulia kuhusu Wabunge, kasema “Wabunge hatufanyi tuliyowaahidi Wananchi” ipo kwenye video hii…bonyeza PLAY kutazama kila kitu!!!