Inaelezwa kuwa Marehemu Rapper Nipsey Hussle ameondoka akiwa bado hajatimiza malengo yake makubwa kwa watu wake. Unaambiwa alikuwa na mpango wa kuboresha makazi ya majirani zake na sio tu waliomzungumka bali mitaa 11 ya watu walioathirika na kimbunga Marekani na Puerto Rico.
Inaripotiwa kuwa aliyekuwa mshirika wa biashara ya Nipsey Hussle, David Gross ametupa habari hizo alipokuwa akizungumza na Los Angeles Times na kusema kuwa Nipsey alikuwa na mpango wa kukutana na viongozi wa ngazi za juu wa watu weusi wa eneo lake ili waweze kukaa mezani na kujadiliana kuhusu mpango aliokuwa nao.
Inatajwa kuwa moja ya mpango mwingine mkubwa aliokuwa nao Nipsey ni kusaidia eneo lake alilokuwa akifanyia biashara, alipanga kuongeza maduka mengine 80 juu ya ghorofa ambalo chini kuna duka lake la nguo (Marathon Clothing Store) ambapo asilimia 20 ya mapato ya kodi alipanga kutumia na wakazi wa eneo lake ikiwemo kuwawezesha kujenga nyumba zao.
VIDEO: Ommy Dimpoz bado anajiuliza “Ni mimi kweli?”, RIP Dr. Mengi