Muziki wa Bongo Fleva unasogea hatua kubwa kila siku, mbali na kutumia TV za Kimataifa kuutangaza muziki mitandao imekuwa ikitumiwa pia kwa asilimia kubwa kuutangaza muziki.
Kuna list ya mastaa waliopata account za VEVO ambazo ni kubwa kwenye kutangaza video za muziki mitandaoni, Baraka Da Prince nae kaingia rasmi kwenye list hiyo, amesema amefurahi kupata akaunti hiyo ambayo itafanya video ya wimbo wake wa ‘Siachani nawe’ ufike mbali zaidi.
255 ilimtafuta Diamond Platinumz ambaye amesema ameshindwa kuwa na account ya VEVO kutokana na wao kumtaka afute account yake ya Youtube aanze upya kwa kutumia akaunti nyingine jambo ambalo hakukubaliana nalo.
Director Kevin Bosco amesema wakati akifanya video ya AY wimbo wa wake wa ‘Asante’ alipata ugumu wa kuifanya kazi hiyo kutokana na models wa video kusumbua ikiwemo kuvunja mkataba na wengine kutokufika, kwa upande wa video ambayo ilikuwa rahisi ni pamoja na ‘Akadumba’ ya Ney Wa Mitego.
Ugumu mwingine uliotokea kwenye video ya ‘Asante’ ni pamoja na Director huyo kuibiwa camera baada ya kuvamiwa na majambazi na kufanya material yote yapotee hivyo kazi ya kushoot ikaanza upya na gharama vilevile zikaongezeka zaidi.
Kusikiliza story zote za kwenye 255 bonyeza play hapa chini…
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook