Unajua hii imekuwa ishu ambayo inakaa sana kwenye headlines, upande wa Bongo Sheria zimebanwa zaidi kuzuia matumizi ya dawa za kulevya, Marekani tukasikia story tofauti, wao kuna Majimbo ambayo yaliruhusu matumizi ya Bangi, uhalali huu umeingiza Bangi kuwa bidhaa halali kabisa kutumiwa na kuuzwa kama ilivyo bidhaa nyingine Majimbo kama ya Washington DC, Alaska, Colorado.
Hii ya leo ni kwamba Jimbo la Colorado unaambiwa wamefanikiwa kukusanya kodi ambayo ni dola Mil. 15 (zaidi ya Bil. 27 Tshs) kutokana na mauzo ya bangi ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.
Fungu hilo la kodi linapelekwa kujenga Shule mbalimbali kupitia mpango wa Jimbo hilo uliopewa jina la Building Excellent Schools Today (BEST)
Tangu kupitishwa utaratibu wa kuruhusu uuzaji wa bangi, unaambiwa maduka ya kuuza bidhaa hiyo rejareja mtaani kuanzia Jan. 1, 2014 mpaka sasa wamefanikiwa kufanya mauzo na kulipa kodi ambayo ni kama dola Mil. 15 ambazo zinasaidia ujenzi wa Shule za Umma katika Jimbo hilo.
Kwako mtu wangu, unadhani itakuwa sawa nchi za Afrika nazo waruhusu bangi ili kuongeza mapato ya kodi?
Kwenye Facebook, Instagram na Twitter natumia jina la millard ayo mtu wangu, jiunge na mimi niwe nakusogezea kila taarifa inayonifikia, kujiunga na mimi bonyeza >>>twitter Insta Facebook