March 20, Miss Singida 2014/15, Doris Mollel alizindua Foundation aliyoipa jina la Doris Mollel Foundation ambayo itakayohusika kukusanya mapato yatakayowasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya kufikisha miezi 9 ‘Watoto njiti’.
Akizungumza kwenye mkutano huo na waandishi wa habari mwenyekiti wa mfuko huo, Doris Mollel amesema lengo la mfuko huo ni kutafuta fedha za kuweza kusaidia jamii katika upande wa watoto njiti ambapo takwimu zilizopo zinaeleza idadi ni ndogo kutokana na jamii nyingine hazina utamaduni wa kwenda kujifungulia katika vituo vya afya hivyo elimu inahitajika kufanya jamii hizi zifike katika vituo vya afya na kuwezeshwa kwa vituo hivyo kuwa na vifaa ili kupunguza vifo vya watoto njiti 9000.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook