Miongoni mwa taarifa zilizochukua Headlines katika taarifa ya Habari ya kituo cha ITV ni hii ya Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima ambae amefika kituo kikuu cha Polisi Dar kwa ajili mahojiano na Jeshi la Polisi kwa madai ya kutoa kauli yenye maneno makali kwa kiongozi wa Kanisa Katoliki, Askofu Kardinali Pengo.
Askofu Gwajima amesema maneno aliyoyatoa ni ya kumkemea kiongozi mwenzake wa kiroho kwa madai ya kukiuka msimamo wa viongozi wenzie wa dini wa kukataa Mahakama ya Kadhi.
“Baraza la Maaskofu Tanzania waliamua kwa pamoja na wakasaini waraka kwa pamoja, kwamba hawataki Mahakama ya Kadhi… lakini tukashangaa mwenzetu Askofu Pengo aliyesaini na yeye anageuka sasa tukajiuliza kwa nini anageuka? mimi kama kiongozi wa kiroho nikaona nimkemee.. lakini nimeitwa na Polisi sasa najiuliza niliyemkemea ni Polisi au nilimkemea nani?“ —Askofu Gwajima.
Hivi karibuni katika mitandao ya kijamii kumezagaa picha za video zenye maneno ya kashfa kwenda kwa kiongozi wa Kanisa Katoliki Askofu Kardinali Pengo jambo lililofanya jeshi la Polisi kumtaka afike kituoni kikuu cha Polisi kwa mahojiano.
Sikiliza taarifa hiyo iliyoripotiwa na kituo cha ITV kwa kubonyeza play hapa chini…
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook