Waziri mkuu msaidizi wa Australia Warren Truss ndio kaitangaza hii, na ni baada ya ajali ya ndege ya Ujerumani kuangushwa kwa makusudi na Rubani msaidizi huko Ufaransa na kuua watu wote ndani yake ambao walikua wanazidi 150.
Truss amesema mashirika ya ndege ya Australia ikiwemo Qantas na Virgin Australia wameanza kuyafanyia kazi mabadiliko ya usalama ambapo kuanzia sasa hakuna cha Rubani kubaki mwenyewe kwenye chumba cha Marubani, kama wako wawili na mmoja akawa anataka kutoka labda kwenda Toilet, inabidi muhudumu mmoja wa ndege aingie kwenye chumba hicho ndio rubani mmoja atoke.
Mabadiliko haya yameanza kufanyiwa kazi toka Jumatatu mchana March 30 2015 ambapo mwanzoni ilikua inaruhusiwa kwa Rubani mmoja kupaki kwenye chumba cha kurushia ndege.
Hii yote imekuja baada ya Rubani msaidizi kwenye ndege ya Ujerumani iliyoanguka Ufaransa kugundulika kwamba aliiangusha ndege kwa makusudi na ni baada ya Rubani mkuu kutoka nje ya chumba cha Marubani, alipotaka kurudi akakuta mlango umefungwa, yaani rubani msaidizi ndio kajifungia na akaiangusha ndege kwa makusudi.