Hekaheka ya leo inatokea Shinyanga inahusu mwanamke mmoja ambae amepanga nyumba toka mwaka 2012, mpaka leo hajalipa kodi.. mwenye nyumba amefanya jitihada nyingi kumdai kodi bila mafanikio.
Mwenye nyumba amesema amemfuata mara nyingi pamoja na kutoa taarifa kwa Mwenyekiti pamoja na Askari lakini hadi leo amekataa kulipa kodi.
Mwanamke huyo anafuatwa na wenye nyumba lakini anakataa kulipa hela hiyo akidai kwamba hao wanaomdai sio wenye nyumba.
Rafiki aliyempeleka kwenye nyumba hiyo alifikishiwa malalamiko hayo, akamfuata lakini bado aligoma kulipa hela hiyo.
Bonyeza play hapa chini kusikiliza Hekaheka yote…
Hakuna Stori itakayokupita mtu wangu,niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza>>> twitter Insta Facebook