Moja ya ishu ambazo zimeleta mvutano mkubwa bungeni ni mjadala kuhusu usajili wa wapiga kura kwa mfumo wa kielektroniki BVR na ishu ya kupigia kura katiba inayopendekezwa.
Jana kulitokea mvutano Bungeni baada ya Mbunge John Mnyika kuomba mwongozo kuhusu changamoto zilizojitokeza kwenye mfumo wa usajili wa BVR.
Taarifa iliyotufikia ni kwamba Mwenyekiti wa ya tume ya uchaguzi Tanzania, NEC Jaji Damian Lubuva ametangaza kuahirishwa kwa mchakato wa kupiga kura ya maoni ya Katiba iliyopendekezwa hadi hapo tarehe mpya itakapotangazwa tena.
Wadau mbalimbali wa siasa wamekua wakitoa maoni yao kuhusu kura ya maoni iliyopangwa kufanyika April 30 huku wengi wakidai ni vigumu zoezi hilo kufanyika kwa wakati kutokana na sababu mbalimbali.
#Stori: Mwenyekiti Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian LUBUVA ametangaza kuahirishwa zoezi la Kupigia Kura Katiba iliyopendekezwa.
— millardayo.com (@millardayo) April 2, 2015
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook