Ajali hii imetokea muda mfupi uliopita eneo la Kinondoni DAR, daladala mbili zimegongana eneo hilo katika Barabara ya Kawawa, katikati ya kituo cha Morocco Hotel na Kinondoni Mkwajuni.. zote mbili zilikuwa zimeongozana kutoka upande wa Kinondoni kuelekea Magomeni.
Askari wa Usalama Barabarani, Thomas L.M ambaye alikuwa eneo la tukio hilo amesema majeruhi wa ajali hiyo ni watu 18 ambao tayari wamefikishwa Hospitali kwa ajili ya matibabu na hakuna mtu aliyefariki.
Askari huyo pamoja na mashuhuda wamesema ajali hiyo imetokana na mwendo wa kasi uliosababisha daladala ya nyuma kuigonga nyingine iliyokuwa mbele yake.
Hapa utawasikia shuhuda wa ajali, dereva wa daladala iliyogongwa na Askari aliyekuwa eneo la tukio.
1. Shuhuda wa ajali hiyo, Mohammed Said.
2. Dereva wa daladala iliyogongwa.
3. Askari aliyekuwa eneo la tukio, Afande Thomas.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook