Katika kipindi cha takribani wiki mbili sasa mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo amekuwa akitawala ‘headlines’ za vyombo vya habari ulimwenguni kutokana na kuimarika kwa kiwango chake katika siku za hivi karibuni.
Wikiendi iliyopita Ronaldo aliweka rekodi ya kufunga magoli 5 bila kuhusisha mkwaju wa penati katika mechi dhidi ya Granada, na jana usiku Ronaldo aliipa tena Real Madrid kwa kufunga goli muhimu dhidi ya Rayo Vallecano – hivyo akawa ametimiza idadi ya magoli 300 akiwa na Real Madrid – hii ni rekodi nyingine katika faili lake, amekuwa ndio mchezaji aliyefikisha idadi hiyo kwa haraka zaidi, ndani ya mechi 288 tu.
Cristiano Ronaldo amekuwa mwiba mchungu kwa karibia kila timu pinzani amewahi kucheza dhidi yake, na leo nakuletea listi ya timu na idadi ya magoli ambayo amewahi kuzifunga timu pinzani katika ligi ya Spain, England, UEFA CUP, na Champions League.
Magoli – Klabu
18 – Sevilla
15 – Atletico Madrid, Barcelona, Getafe
14 – Atletico Bilbao
13 – Malaga
12 – Celta Vigo, Levante
11 – Villarreal, Granada
10 – Osasuna
9 – Aston Villa, Valencia, Rayo Vallecano, Real Sociedad, Deportivo
8 – Tottenham
7 – Schalke, Ajax, Zaragoza, Mallorca, Elche, Almeria, Fulham, Wigan
6 – Racing Santander, Galatasaray, Arsenal, Bolton, Newcastle, Portsmouth
5 – Everton, Manchester City, West Ham, Middlesbrough
4 – Bayern Munich, Marseille, Lyon, Xerez, Espanyol, Derby, West Brom, Reading
3 – FC Copenhagen, Borussia Dortmund, Roma, Juventus, CSKA Moscow, Real Betis, Valldolid, Dinamo Moscow, Liverpool, Blackburn
2 – Ludogorets, AC Milan, Sporting Lisbon, Basle, Zurich, Eibar, Gijon, Hercules, APOEL, Southampton, Birmingham, Stoke, Hull, Manchester United, Watford
1 – Auxerre, Inter, Gamba Osaka, Porto, Murcia, Tenerife, Cordoba, Ponferradina, Debreceni, Sunderland, Charlton, Chelsea, Millwall, Exeter