Premier Bet SwahiliFlix Ad Halotel Ad

Stori Kubwa

Ajali ya April 9 2015 Tanga, Mabasi mawili yamegongana na chanzo ni hili gari dogo.

on

aj 1Tangu ilipotokea ajali ya barabarani eneo la Changarawe Iringa ambayo ilitokana na basi la abiria la Kampuni ya Majinjah Express kugongana na lori, stori zikaendelea kuwa nyingi kwenye vyombo vya habari, nyingi zikiandikwa kuhusu vyanzo vya ajali hizo.

Ajali nyingine tena imetokea Tanga leo APRIL 9 2015, taarifa za awali zinasema watu 10 wamefariki na wengine wamepata majeraha kutokana na ajali hiyo iliyotokea eneo la Mkata, Wilaya ya Handeni Tanga, gari zilizopata ajali hiyo ni basi la NGORIKA, jingine la RATCO pamoja na gari nyingine ndogo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, RPC Juma Ndaki kathibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akisema kwamba mwendo kasi umechangia kutokea ajali hiyo.

Hizi ni PICHAZ ambazo zimeenea mitandaoni zikionesha jinsi hali ilivyo eneo la tukio.

IMG-20150409-WA0014 IMG-20150409-WA0015

IMG-20150409-WA0016

IMG-20150409-WA0017

IMG-20150409-WA0018

IMG-20150409-WA0013

IMG-20150409-WA0019#RIP kwa watu wetu waliofariki kwenye ajali hiyo, pole kwa waliopata majeraha pia.

millardayo.com ni sehemu yako utakapozipata zote unazozitaka, vichekesho, stori za siasa, muziki, michezo, movies, magazeti, video mpya na nyingine kubwa….  unaweza kujiunga na mimi Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook

Soma na hizi

Tupia Comments