Kama kuna kitu kinasubiriwa kwa hamu na wanaolipenda soka duniani ni mechi ya mahasimu wa jadi wa jiji la Manchester matajiri wa Manchester City dhidi ya Manchester United weekend hii.
Kwa miaka mingi rangi nyekundu imekuwa ikitawala hili jiji lakini lakini katika kipindi cha miezi 16 iliyopita hali imekuwa tofauti, rangi ya blue imekuwa ikitawala jiji.
Hata hivyo kwa mara ya kwanza tangu November 23 2013, Manchester United wataikaribisha City Old Trafford wakiwa wapo juu ya Manchester City kwenye msimamo wa ligi kuu ya England wakiwa wamecheza idadi sawa ya mechi.
Mara ya mwisho kwa Man United kuwa juu ya City kwenye msimamo wa ligi ilikuwa baada ya mechi 11 katika msimu wa 2013/14 wakiwa chini ya Sir Alex Ferguson ambapo United walikuwa mbele ya City kwa pointi 1 kwenye msimamo.
Jumapili hii timu hizo zinakutana Old Trafford huku Manchester United wakiwa mbele kwenye msimamo wa ligi kwa pointi 62 na wapinzani wao City wakiwa na pointi 61.