Cha mwisho kusikika kutoka kwenye HEADLINES za Bungeni March 2015 ilikuwa ishu ya mjadala wa Muswada wa Matumizi ya Mtandao, mvutano ukawa mkubwa na kusababisha Bunge kuahirishwa saa tano usiku… Wabunge walikuwa wakivutana kuhusu kupitisha baadhi ya vipengele kwenye Muswada huo.
Okay, n’na stori ya Kenya sasa hivi, ishu ni hiyo hiyo kesi ya matumizi ya mitandao.. Kijana mmoja Robert Mungai yeye tayari yuko mikononi mwa Mahakama, kinachosubiriwa ni Mahakama kuendelea kusikiliza kesi yake na kuamua hukumu pia kutokana na jamaa huyo kukabiliwa na kesi ya kuandika ujumbe wa uongo kwenye ukurasa wake wa Facebook siku ya April 4 2015.
Polisi Kenya wamesema Robert aliandika ujumbe wa kuwaonya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Egerton University kilichoko Njoro, ambapo ujumbe alioandika alikuwa akiwataarifu wenzake kuwa Kikundi cha Al-Shabaab kitashambulia.
Robert alikataa kutenda kosa hilo lakini Polisi walikataa asiachiliwe kwa dhamana kwa kuwa uchunguzi bado haujakamilika.
Imeripotiwa na vyombo vya habari Kenya, wanasema kwa Sheria ya nchi hiyo ilivyo huenda hukumu yake ikawa kifungo cha zaidi ya miaka ishirini.
Alan Wadi Okengo aliwahi kuingia kwenye HEADLINES pia toka Kenya January 2015 baada ya kuhukumiwa mwaka mmoja jela na kulipa faini kwa kosa la kumtukana Rais Kenyatta mtandaoni.
Ilisikika kwenye show ya #AMPLIFAYA.. TV ya K24 waliripoti hii pia, unaweza kuisikiliza na kuangalia video yake hapa…
millardayo.com ndio sehemu yako kuzipata story zote mtu wangu, unaweza kuwa karibu zaidi na mimi kwa kujiunga kwenye Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook