Kuna ishu ambayo ukiisikia kwa mtu anasimulia unaweza kuichukulia poa yani.. lakini ukikutana na story kamili lazima ukae vizuri kuisikiliza ishu ikoje.
Hii nimekuta kwenye mtandao wa gazeti maarufu Uingereza, linaitwa The Independent.. wameandika ripoti inayoonesha kwamba kuna kundi kubwa sana la Wanajeshi wa Uingereza ambao wamegundulika kuumwa ugonjwa wa akili, sababu ya ugonjwa huo ni dawa ambazo huwa zinatumiwa na Wanajeshi hao ili kuzuia wasipate maambukizi ya Malaria !!
Dawa hizo zinaitwa Mefloquine au jina jingine Lariam.. tayari toka 2008 mpaka leo kuna wanajeshi karibu 1,000 ambao walipata matatizo ya akili kutokana na kutumia dawa hizo wakiwa nje ya Uingereza kupigana vita.
Athari nyingine baada ya kutumia dawa hizo ni pamoja na kupata stress, na wengine wanajiua kabisa!
Alastair Duncan ni Meja Jenerali Mstaafu wa Jeshi hilo ambae aliwahi kwenda kwenye vita Sierra Leone, yeye ni mmoja ya walioathirika kwa kupata tatizo la akili baada ya kutumia dawa hizo.
Sasa ishu iko hivi, tunajua wanajeshi wakiwa kwenye kazi yao huwa wanakuaje, vipi unakutana nao wakati tayari wameathiriwa na dawa hizo?