Najua maswali yalikuwa mengi kwa watu kuhusu kinachoendelea Afrika Kusini.. tuna ndugu zetu, jamaa.. marafiki walioko ndani ya nchi hiyo.. kusikia ishu ya mauaji ya raia wa kigeni walioko ndani ya nchi hiyo lazima ikushtue.
Waziri Membe kato majibu kuhusu kinachoendelea huko, huenda umeona post za alichokisema mitandaoni, hapa nimenukuu na kukuwekea sauti yake mwenyewe>>Katika mgogoro huu hatujapoteza Mtanzania hata mmoja.. nimehakikishiwa.. tuna Watanzania wamekufa watatu.. yupo Marehemu Rashid Jumanne ameuawa kilometer 90 kutoka Durban.. aliuawa akiwa kwenye kitendo cha unyang’anyi, Polisi wameuhifadhi mwili wake kwa ajili ya Postmortem.>>
>>Yupo marehemu Athuman China ‘Mapepe’.. huyu ameuawa kwa kupigwa visu ndani ya gereza lililopo Durban, alikuwa amefanya makosa ya jinai akahukumiwa kwenda jela, akiwa jela kukazuka mapigano ya wafungwa ambapo kadhaa walijeruhiwa na Mtanzania huyu alikuwa miongoni mwa waliigwa visu, na baadae akafariki>>
Tatizo la Xenophobia ni jambo ambalo halitakiwi.. halikubaliki.. na linatakiwa kulaaniwa kote duniani. Linapohusu mauaji hata kama ni mtu mmoja amekufa, Tanzania inalaani suala hili..“>> Waziri Bernard Membe.
Unaweza kumsikiliza hapa Waziri Membe..
Hakuna Stori itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook