Story za India mara nyingi huwa zinanishtua kidogo.. ni hukohuko ambako bwana harusi alimkataa bibi harusi siku ya ndoa, ndoa ikavunjika kwa sababu hakumvutia.. ni hukohuko bibi harusi alifunga ndoa na mgeni rasmi baada ya mume wake mtarajiwa kuanguka kwa kifafa siku ya ndoa.. ziko nyingi sana ishu za vioja vya India, leo n’na nyingine.
Eti mume wa mwanamke mmoja ametoroka na mke wa jirani pamoja na watoto wawili wa jirani huyo, hii kesi ikasogezwa kwenye meza ya Baraza la Kijiji, Baraza likaamua kwamba mwanamke huyo anatakiwa kulipa faini ya hela ya India ambayo ni Rupee laki 3, ambayo Bongo ni kama Mil.9 hivi.. kama akishindwa kulipa faini hiyo basi inabidi akubali kuolewa na jamaa ambae mke wake ametoroshwa na mumewe.
Mwanamke ambaye kapewa hukumu hiyo anaitwa Mamta, mume wake aliyetoroka na mke wa jirani ni Kalulal.. Rajendra Meghwal nd’o mwanaume aliyepeleka madai yake Baraza la Kijiji kudai fidia ya kutoroshewa mkewe.
Polisi wamesema wanachunguza hii ishu, japo Mamta ambae anatakiwa kulipa fidia hakuwepo kwenye kikao kilichotoa hukumu hiyo.
Mara nyingi ishu za namna hii huwa maamuzi yanayotolewa yanakuwa yakilalamikiwa sana kutokana na kwamba Mabaraza ya Wazee ya vijiji huwa wanajifanyia maamuzi ambayo mengine ni kinyume na haki za binadamu.
Hii hukumu aliyopewa huyu mwanamke iko sawa kweli?