Hii ni sehemu ya tatu ya ile Hekaheka ya mwanamke mmoja aliyeenda kuolewa kwa mara ya pili lakini ndoa hiyo ikazuiwa baada ya story kuvuja kwamba mwanamke huyo alikuwa anaolewa kwa mara ya pili.
Jana alisikika mume wa mwanamke huyo ambapo alisema hawakuwahi kuwa na ugomvi katika ndoa yao ila alishangaa kuona mke wake anadai talaka ghafla bila sababu, baadae akasikia kwamba ameolewa na mwanaume mwingine.
Leo amesikika mwanamke huyo ambaye alitoka kwa mumewe na kwenda kuolewa mara ya pili, amesema walikuwa na mgogoro na mume wake wa kwanza wakaachana.. baadae akakutana na mwanaume wa pili, alihisi huyu ni kama anamdanganya.. wakaendelea na uhusiano baadae mwanaume huyo akamwambia kwamba anataka kumuoa, akaona akimwambia ukweli atamkataa.
Ishu ikamfikia mume wa kwanza, akaanza kumtafuta mwanaume huyu ambaye anamuoa mke wake na kumfanyia fujo.
Amesema ni kweli alikosea na yuko tayari kumuomba msamaha mwanaume anayemuoa mara ya pili lakini hayuko tayari kurudiana na mwanaume aliyemuoa mara ya kwanza.
Kusikiliza muendelezo wa Hekaheka yote bonyeza play hapa chini..
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter,Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa>>>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.