Baada ya Bayern Munich na FC Barcelona kutangulia kuingia katika hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya April 21 2015, April 22 ilikuwa zamu ya club nyingine mbili kuungana nao.
Jijini Madrid Spain, Real Madrid wakiwa Santiago Bernabeu walikuwa wakitetea ubingwa wao wa Ulaya kwa kucheza dhidi ya wapinzani wao Atletico Madrid ambapo ilikua ni mechi ya pili baada ya mechi ya kwanza kutoka sare tasa.
Tofauti na ilivyokuwa kwa mchezo uliopita safari hii Madrid wakiwa na upungufu wa wachezaji muhimu wamefanikiwa kupata ushindi wa 1-0 na wanazitoa shukrani kwa kijana wa kimexico Javier Hernandez Chicharito aliyefunga goli la ushindi dhidi ya Atletico na kuipeleka Madrid katika nusu fainali ya 37 ya michuano hiyo.
Kwenye mechi nyingine pia Juventus ya Italia imefanikiwa kuingia nusu fainali baada ya kupata ushindi wa jumla dhidi ya Monaco.
Kwa matokeo hayo FC Barca, Bayern Munich, Real Madrid na Juventus ndio timu nne zilizoingia kwenye nusu fainali ya UCL na ratiba ya mechi zao itapangwa rasmi Ijumaa wiki hii.