Jumatatu ya April 27, tayari Magazeti ya leo yapo mtaani, POWERBREAKFAST ya CLOUDS FM nayo imeshafanya uchambuzi wa stori zote.. hapa unaweza kuzisoma na kuzisikiliza pia…
Rais Kikwete ametoa msamaha kwa wafungwa 4,129 katika maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano, Mwalimu mkuu Lindi amekuta jeneza limewekwa mlango wake, watu wanaodhaniwa kuwa majambazi wamefukua kaburi Kibaha na kuiba vitu alivyozikwa navyo marehemu, SUMATRA na Jeshi la Polisi kuanza ukaguzi wa mikataba ya madereva wa mabasi na malori, wizara ya mambo ya ndani inatarajia kufuta taasisi 24 kwa kushindwa kuwasilisha taarifa za ukaguzi.
Imesikika stori ya Mbunge wa Ubungo John Mnyika ambae amemtaka Spika wa Bunge kuitisha kwa dharura kamati ya kudumu ya katiba, sheria na utawala, Watanzania 26 wamerejea TZ kutoka Afrika Kusini, waliokuwa wakimbizi zaidi ya 152,000 walioingia TZ mwaka 1972 wamekabidhiwa vyeti vya uraia wa Tanzania na ghasia zimeibuka Burundi kati ya maafisa wa Polisi na waandamanaji.
Kwenye uchambuzi huo kulikuwa na mazungumzo na Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Serikali Mindi Kasiga ambae amezungumzia Watanzania 26 waliorejea TZ kutoka Afrika Kusini na hali ya waliobaki kwenye kambi ya muda nchini humo pia kulikuwa na mazungumzo na mfatiliaji wa mambo ya siasa Dr. Benson Bana akizungumzia hali ya kisiasa inayoendelea nchini Burundi.
92.9 Clouds FM inasikika ukiwa Iringa.
Bonyeza play kusikiliza uchambuzi wote wa Magazeti ya leo April 27..
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook