Yanga Bingwa 2014/2015!! Hizi ni baadhi ya headlines kwenye kurasa za michezo.. haikumaanisha kwamba matokeo ya mwisho yalikuwa yameamua hvyo, ila wanspoti walipiga hesabu ya pointi ambazo yatari YANGA walikuwa wamejikusanyia mpaka mechi yao ya mwisho, hii ya leo ambayo Yanga wamekutana na Polisi Morogoro tayari imetoa matokeo.
Yanga imefikisha jumla ya pointi 55 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote inayoshiriki ligi kuu msimu huu, kwa matokeo hayo basi Yanga wanakuwa mabingwa wa Ligi hiyo.
Mechi hiyo kati ya Yanga na Polisi Moro ilikuwa ikipigwa katika Uwanja wa Taifa Dar.. mechi imekamilika kwa Yanga kutoka kifua mbele kwa goli 4-1.
Hamis Tambwe leo aliweza kuing’arisha Yanga baada ya kupachika magoli matatu ambapo goli la kwanza alifunga dakika ya 40 kufuatia krosi ya Saimon Msuva, goli la pili alilifunga dakika ya 53 na goli la mwisho alifunga baada ya kupokea cross kutoka kwa Mrisho Ngassa.
Msuva alikamilisha idadi ya mabao kwa kupiga bao la nne ambapo baadae dakika ya 83 Polisi walishinda bao la kufutia machozi kupitia kwa Bantu Admini aliyepiga shuti kali akiwa nje ya 18.
Ligi kuu Tanzania Bara inatarajiwa kukamilika mwisho wa wiki katika mechi za kukamilisha ratiba ya ligi hiyo kwa msimu huu.
#LiveMATCH – Ligi kuu TZ Bara Yanga SC 2-0 Polisi Moro
— millardayo.com (@millardayo) April 27, 2015
Msuvaaaaaa imoooo. Yanga 4-0 Polisi. #VPL2015
— Vodacom Tanzania (@VodacomTanzania) April 27, 2015
Full Time: Yanga 4-1 Polisi Morogoro ( Tambwe 3x, Msuva| Admini Bantu) #VPL2015 Yanga ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
— Vodacom Tanzania (@VodacomTanzania) April 27, 2015
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenyeTwitter,Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa>>> TwitterInstaFB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribeYouTube kwa kubonyeza hapa>>>>Videos ili kila video ya AyoTVikufikie.