Stori ambayo kwa sasa imechukua headlines kwa wingi ni ile ya tetemeko la ardhi lililotokea Nepal na kuua idadi kubwa ya watu karibu na milima ya Everest.
Idadi ya watu ambao wamethibitishwa kufariki kutokana na tetemeko hilo lililotokea siku ya jumamosi iliyopita imeongezea na mpaka sasa ni watu zaidi ya 4,500 waliofariki.
Serikali ya nchi hiyo imesema zaidi ya watu 10,000 wamejeruhiwa.. Hali hiyo imewaelea na Serikali imehitaji msaada kutoka mataifa mengine.
Waziri Mkuu wa Nepal, Sushil Koirala amesema mahitaji ya dharura yanayohitajika yakiwa ya mahema , chakula pamoja na maji.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>>Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.