Mbali na uwezo wake mkubwa wa kumiliki mpira uwanjani, Didier Drogba raia wa Ivory Coast amekuwa na mchango mkubwa katika shughuli za kijamii ambazo ambazo amekuwa akishiriki ndani ya nchi yake na Afrika pia.
Uongozi wa ligi kuu ya England FA umeridhishwa na kazi yake.. wameamua kumpa tuzo kutokana na mchango wake mkubwa wa kuhamasisha soka la vijana Afrika na uamuzi wake wa kufungua Didier Drogba Foundation ambayo itakuwa ikifanya kazi ya kuwasaidia watu wenye mahitaji mbalimbali.
Staa huyo wa soka wa Chelsea amepewa heshima hiyo kama sehemu ya kumpongeza kwa kazi nzuri za kijamii anazofanya.
Tayari Drogba amejenga hospitali kubwa ya kisasa nchini kwao Ivory Coast.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.