Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Kwa mara ya kwanza Zari na Diamond Live kwenye Interview on @CloudsFM na Clouds TV (PICHAZ)

on

IMG_4056Ilikuwa Exclusive.. LIVE kupitia #Superbrand Radio @CloudsFM na Clouds TV pia, leo usiku headlines zitakuwa na mengi kutoka kwenye burudani ya #ZariAllWhiteParty pale Mlimani City Dar.

Kwa mara ya kwanza hii ilikuwa interview ambayo iliwakutanisha wote wawili kwa pamoja, Zari na mpenzi wake staa wa muziki, Diamond Platnumz.

Kwenye interview hiyo kuna haya majibu ya ishu ambazo huenda hukuwahi kuzisikia wakiongelea kokote.. nimeona nikusogezee kama ulikuwa mbali na TV na radio yako yako mtu wa nguvu na wewe usipitwe.

<<Mara ya kwanza ilikuwa kwenye social network tu.. nilikuwa namuonaona tu napita kwenye page yake na-like.. nilitoka kushoot video ya ‘Coco Baby’ South Africa tukakutana kwenye ndege..>>Diamond Platnumz anasimulia walivyokutana na mpenzi wake Zari kwa mara ya kwanza.

IMG_4056Kumbe hiki ndicho kilimvutia sana Zari kwa Diamond Platnumz>>Ni mchangamfu.. anajali.. Diamond ana akili sana, nilivutiwa nae kwa sababu ana akili sana.. anajituma sana, ni mtu mwenye malengo makubwa..>>Zari.

Kwani Diamond amewahi kuonana na watoto wa Zari?? Wanamchukuliaje? >>Bado hawajawahi kuonana.. ila watoto wanamjua.. kama mama yao nina furaha wao wana furaha pia>>—Zari.

Hivi ndivyo Diamond alivyomzungumzia Zari pamoja na maisha yao >>Anajua kuna maisha ya kwenye media na kuna maisha ya ukweli.. Japokuwa watu wanahisi vitu vingi viko kwenye public, ni uongo.. tuna maisha ya social media na tuna maisha private..>>

<<Sitembeagi na washkaji.. kila mtu yupo na kila mtu analipwa kutokana na kazi yake.. kila mtu yuko kikazi kabisa na tumekutana katika kazi..>> Hapa Diamond alikuwa anazungumzia kundi la watu ambao huwa anaongozana nao mara nyingi.

Zari ni wa Uganda na Diamond ni Mtanzania, wapi wameamua kuweka makazi yao rasmi >> “ Tutaishi hapahapa.. kwa utamaduni wetu inabidi mwanamke uondoke nyumbani kwenu umfuate mpenzi wako mkaishi wote.. Watanzania ni watu poa sana siwezi hata kuwalinganisha.. ni wakarimu sana.>> Zari.

Pichaz 13 kutoka kwenye interview hiyo unaweza kuzcheki hapa.

IMG_3977

.

IMG_3981

.

IMG_4045

Diamond na Zari wakiwa wanafika kwenye studio za Clouds Media. Nyuma yao kuna support ya nguvu ya mabaunsa wao.

IMG_4056

IMG_4060

IMG_4065

Mtangazaji Gerald Hando anasalimiana na Zari.

IMG_4106

IMG_4144

IMG_4185

Mkono wa kushoto wa Zari unaonekana na pete, ndiyo kusema shughuli tayari kweli??

IMG_4192

Le Mutuz, mmoja ya Bloggers TZ

IMG_4242

IMG_4258

Diamond na Zari wanapiga picha na wanafamilia wengine wa Clouds FM.

IMG_4284

Baada ya kumaliza Diamond na Zari waliondoka kwenye BMW, gari la msanii Diamond Platnumz.

Watu wategemee show kubwa kutoka kwa AKA, Shetta na wasanii wengine.. hili ni tukio kubwa sana la kuenjoy.. watu wanafanya sana kazi na hawajui jinsi ya kupunguza stress, White Party ni event kwa ajili ya kula good time” >> Zari.

Show iko baadae pale Mlimani City watu wa nguvu, kila kitakachotokea utakipata pia hapahapa millardayo.com.

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments