Ni siku moja tu imepita tangu Bayern Munich ilipofungwa na Barcelona kwenye mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya ligi ya mabingwa, mzigo wa lawama za kufungwa kwa Bayern umesukumwa kwa kocha wa Klabu hiyo, Pep Guardiola.
Guardiola amejikuta akibebeshwa lawama za kipigo hicho na magazeti ya kila siku ya Ujerumani, ambapo gazeti Bild lilikuwa na Headline>>‘Guardiola amefungwa na Barcelona na hakukuwa na muda wa kumbukumbu nzuri ya kurudi kwake nyumbani kwao Barcelona’>>
Story ikaendelea na mlolongo wa lawama kwa kocha huyo>> ‘Barca ilimuonyesha kocha huyo udhaifu alio nao’.
Gazeti hilo lilikumbusha vipigo vingi vya Bayern>> 3-0 cha 3-0 dhidi ya Borrusia Dortmund , 4-0 dhidi ya Real Madrid na 4-1 dhidi ya VFL Wolfsburg >> mwisho wa story kukawa na swali kwamba ataweza kugeuza kipigo hiki???
Gazeti lingine la kila siku la Die Zeit liliandika kuwa Bayern na Pep Guardiola kwa pamoja wamepewa darasa la jinsi ya kucheza soka katika mchezo huo.
Gazeti la Kicker limekwenda mbali zaidi kwa kuandika kuwa hiki kilikuwa zaidi ya kipigo na kwamba matokeo hayo yamemuacha Guardiola akiwa amepigwa butwaa.
Wachezaji wengi wa zamani nchini Ujerumani walilalamikia mbinu zilizotumiwa na Pep Guardiola kwenye mchezo huo, akiwemo kipa wa zamani Oliver Kahn ambaye alilaumu jinsi ambavyo Bayern ilishindwa kujilinda na kuizuia Barcelona isifunge.
Katika mchezo wa jana Bayern Munich ilifungwa 3-0 baada ya Lionel Messi kufunga mabao mawili na kutengeneza bao lingine lililofungwa na Neymar na kuiacha Bayern Munich ikiwa hatarini kutolewa kwenye nusu fainali kwa msimu wa pili mfululizo.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.