Siku ya Jumapili May 10 2015 kutakuwa na show kubwa pale Maisha Club Dar, ambapo staa wa muziki rapper Mabeste ameandaa show ambayo ameipa jina la ‘MRS MABESTE Charity Show‘.
Ishu ya mke wa Mabeste kuumwa imeanza kusikika muda mrefu, kuna kiasi cha pesa ambacho kinatakiwa kipatikane ili Mrs. Mabeste apate matibabu.. Leo Mabeste alikuwa kwenye show ya Leo Tena, amezungumzia juu ya show hiyo ambayo wasanii zaidi ya 40 wa Bongo wamejitolea kufanya show hiyo ili pesa zitakazopatikana zimsaidie kwenye matibabu.
List ya mastaa ni kubwa, kuanzia Bongo Fleva, Bongo Movie.. mtu wako wa nguvu nitakuwepo pia, nitafurahi kuona support yako kwa mtu wetu ili tupate mchango Mrs. Mabeste apatiwe matibabu.
Mastaa watakaokuwepo kwenye hii show wengine unaweza kuwacheki kwenye ukurasa wake Instagram hapa >>@mabeste_tanzania
Msikilize Mabeste kwa kubonyeza play hapa..
Kingine ambacho nimekisikia Exclusive kwenye Leo Tena kumbe Mabeste ndio aliyeandika wimbo wa Sisikii wa Jux !!>>”Kipindi fulani aliumwa, Jux alikuwa anataka nyimbo nikaandika ile #Sisikii, theme nzima niliitoa kwenye maisha ya mke wangu.. Sisikii ile ya Jux mwandishi ni mimi.. nikawa nimemwambia kabisa nimemwandikia Jux nyimbo lakini hii nyimbo ni yako, ningekuwa mwimbaji ningeiimba”– Mabeste.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.