Hii ni mara ya pili kwa nchi ya Nepal kukumbwa na tetemeko la ardhi ambalo linadaiwa kuua zaidi ya watu 40 huku kukiwa na idadi kubwa ya majeruhi na kuacha watu wakiwa na hofu ya maisha yao na kuishi kwa mashaka makubwa.
Mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo hakuwa nyuma baada ya kuguswa na kinachoendelea nchini humo na kuamua kutoa mchango wake kwa ajili ya kusaidia waliopatwa na maafa.
Ronaldo ametoa sehemu ya fedha zake pauni milioni 7 ilikusaidia walioathirika na tetemeko hilo la ardhi.
April 25 kulitokea tetemeko la ardhi lililoua zaidi ya watu 8000 huku maelfu ya watu wakikosa sehemu za kuishi.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyezahapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahaukusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTVikufikie.