Uchaguzi mkuu wa kumpata Rais mpya wa Shirikisho la soka duniani FIFA unatarajia kufanyika May 29 huku wagombea wakiwa katika maandalizi ya mwisho kabla ya uchaguzi huo kufanyika.
Wakati zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kufanyika habari mpya ni kuhusu mgombea wa kiti hicho Michael Van Praag kujiondoa kwenye kinyang’anyiro.
Kujiondoa kwaRais huyo wa shirikisho la soka la Uholanzi sasa kumewaacha wagombea wawili pekee wanaowania kiti hicho pamoja na rais wa FIFA Sepp Blatter.
Van Praag, amesema ameamua kujiondoa bila kushinikizwa na mtu na sasa atamuunga mkono mgombea Urais Prince Ali Bin Al-Hussein wa Jordan katika uchaguzi huo.
Wagombea wengine wanaowania nafasi hiyo ni mchezaji wa zamani kiungo kutoka Ureno Luis Figo pamoja na Rais aliyeko madarakani kwa sasa Sepp Blatter ambaye anapewa nafasi kubwa ya kushinda ikiwa ni muhula wake wa tano.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.