Mara nyingi waandishi wa habari wamekuwa wakishutumiwa kwa kaucha taaluma zao na baadhi kujiingiza kwenye mambo ya kisiasa kwa kuandika habari ambazo zina lengo la kupotosha jamii.
Hivi karibuni Waandishi wa habari kutoka Misri walikaa kwenye Headlines kwa muda mrefu baada ya kuhukumiwa kwa kosa la kushirikiana na kundi la Muslim Brotherhood na kuandika habari za kichochezi.
Stori nyingine iliyonifikia leo inatokea huko Niger ambapo mwandishi wa habari mmoja ameshtakiwa kwa kosa la kushirikiana na kundi la kigaidi la Boko Haram.
Waziri wa mambo ya ndani wa Niger alisema mwandishi huyo Moussa Tchangari amekuwa akishirikiana na kundi hilo la kigaidi na kueneza taarifa za uongo ambazo zilikua na lengo la kuchochea vurugu.
Pia amekuwa mstari wa mbele kuandika habari zisizo za kweli kuhusu jeshi la nchi hiyo akidai lina makosa na si Boko haramu huku mapema mwezi huu aliandika habari za kichochezi.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.