Kwa sasa Rais wa FIFA Sepp Blatter hana mpinzani baada ya wagombea wenzake wanaowania nafasi hiyo kujiondoa kwa madai uchaguzi huo umegubikwa na rushwa zaidi badala ya haki.
Uchaguzi huo umepangwa kufanyika kufanyika May 26 mwishoni mwa juma hii huko jijini Zurich, Uswis.
Baadhi ya wadau wa soka duniani wamekua na mitazamo hasi kuhusiana na Rais huyo kuendelea kuongoza Shirikisho hilo kwa mara nyingine huku mkongwe wa soka kwa mara nyingine Maradona akimvaa Sepp Blatter kwa kumuita kuwa ni kiongozi wa mabavu.
Kauli ya Maradona imekuja baada ya FIFA kutengeneza mazingira mazuri ya Rais huyo kuongoza tena na kudaiwa kuwepo mazingira ya rushwa ambayo mwenyewe ameyaita ni ya udhalilishaji.
Alisema kwa miaka ya sasa mchezo wa mpira wa miguu umebadilika na kujaa siasa pamoja na rushwa na FIFA wamekua wakiukandamiza kwa kuendekeza rushwa kwa kiasi kikubwa.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.