Kwenye Hekaheka leo MAY 25 2015 inahusu ishu ya mwanamke mmoja kulalamika kuwa mume wake ana uhusiano na mwanamke mwingine nje.. hii ilimkwaza kwa kipindi kirefu na alipomwambia aachae nae anamdanganya kwamba wameachana lakini uhusiano wao unaendelea chinichini.
Siku moja alikuta simu ya mwanamke huyo imesahaulika kwenye gari ambayo alikuwa nayo mume wake, akaamua kumtafutia watu wa kwenda kumsema kutokana na tabia hiyo.
Mwanamke huyo aliamua kwenda na watu hao mpaka Kimara ambako mwanamke huyo mwenye uhusiano na mumewe anafanya shughuli zake.. baada ya kufika na kundi hilo la watu, mwanamke huyo alishtukia akakimbia.. watu wakaanza kumkimbiza.
Hekaheka ikaishia kwenye nyumba ambayo mwanamke huyo alijificha, wakabaki wanampigia ngoma na kumuimbia kwamba anachukua waume za watu lakini mwanamke huyo alijificha wala hawakumkamata.
Hekaheka iko yote hapa, ukiplay utasikiliza yote iliyosikika leo kwenye #LeoTena @CloudsFM
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.