Wikiendi iliyopita kulikuwa na event kubwa Mbeya ambapo wanafunzi wa Chuo cha Mzumbe waliamua kufanya Tanzania College Star Music ili kusaka vipaji vya wanafunzi wa waliopo vyuoni.
Godlove Msigwa ambaye ni mmoja ya waandaaji wa event hiyo amesema washindi wa Mbeya tayari wamepatikana na event itafanyika mikoa mbalimbali TZ.. mpango walionao ni kuisogeza event hiyo baadae kuwa TV show itakayokuwa ikionesha maisha ya wanafunzi vyuoni.
Ijumaa na Jumamosi ilikuwa weekend yenye matunda poa kwa presenter wa show ya Take One @CloudsTV… Zamaradi Mketema alishinda Tuzo siku ya Ijumaa katika Tuzo za Watu na siku ya Jumamosi pia kwenye Tuzo za Filamu TZ… Zamaradi amesema ushindi wa Tuzo hizo umempa nguvu ili kufanya kazi ya movie nyingine ambazo zitakuwa nzuri zaidi.
Kulikuwa na mabishano kwenye mtandao wa Instagram kati ya Diamond Platnumz na mwanamitindo mmoja wa Marekani ambae alilalamika kwamba Diamond alivaa shati ambalo ni kazi ya designer huyo lakini lilikuwa feki.
Diamond amesema waliona ishu yenyewe haimhusu yeye kwa sababu hakuangalia kama shati ni original au feki, aliliona akalipenda na akaamua kununua.. kama halikuw original designer hakupaswa kumfuata yeye kumlamu.
255 iko kwenye hii sauti hapa, ukiplay utasikiliza hizo story zote