Dubai ni moja kati ya miji inayokua kwa kasi sana duniani. Na ni miongoni mwa miji ambayo inafahamika kwa majengo ya kipekee na kifahari huku watu wengi kutoka sehemu mbali mbali duniani wakivutiwa kwenda Dubai kutalii ama kufanya biashara.
Kwenye headlines leo ni mpango wa kuboresha michezo nchini humo, ambapo unaambiwa wameaamua kujenga uwanja wa kisasa wa mchezo tennis chini ya bahari.
Dubai wako kwenye mkakati wa kutekeleza project yao mpya unaojulikana Underwater Tennis Stadium itakayowezesha mashabiki wa mchezo wa tennis Dubai na duniani kuenjoy kucheza au kushuhudia mechi za tennis chini ya maji.
Krzysztof Kotala ndio msanifu majengo mkuu anaehusika na ujenzi wa uwanja huo wa chini ya maji na anasema anataka uwanja uwe zaidi ya uwanja wa michezo kwani utakuwa na sehemu ya vivutio vya kitalii kwa watu wanaopenda kwenda Dubai kwa matembezi yao binafsi.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.