Alisikika Rapper Young Dee kwenye #255 ya jana JUNE 02 2015 akisema anaandaa video ya wimbo wa Cowbama na kwenye video ataonekana jamaa ambae kafanana sana na Marehemu Albert Mangwea.
Ngwea Junior amesema aliipokea kwa furaha taarifa ya kwamba Young Dee atamshirikisha kwenye video hiyo, anaamini kwamba hiyo ni moja ya njia zitakazomsogeza kwenye mafanikio makubwa ambayo amelenga kwenye maisha yake.
Mkubwa Fella na Babu Tale wako mzigoni, sasa hivi wako kwenye maandalizi ya TV show ambayo itaitwa ‘Kalia Kiti‘.. Babu Tale amesema hii show itakuwa na vitu vingi ikiwemo story za wasanii, muziki ulivyokuwa zamani, mbali na hivyo itakuwa pia show ambayo itawaleta watu karibu zaidi na mtaa na kujua vitu vingi vinavyoendelea.
Story ya mwisho yuko Rapper mwingine anayewakilisha Rock City, Mwanza TZ.. Fareed Quincy Kubanda aka Fid Q ambae yuko kwenye list ya wakali watakaoiwakilisha TZ kwenye msimu mpya wa Coke Studio, Nairobi Kenya.
Fid amesema ni furaha nyingine kubwa kwake kushare jukwaa na Maurice Kirya kwa kuwa muunganiko wao utatoa Fleva nyingine kali ya muziki.. Fid amesema wanafahamiana muda mrefu na Maurice kwa hiyo kazi haitokuwa ngumu safari hii.
255 iko kwenye hii sauti hapa, ukiplay utasikiliza story zote.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.