Stori ya Msiba wa aliyekuwa Sheikh Mkuu Tanzania, Mufti Sheikh Issa Shaaban Bin Simba imechukua nafasi kubwa sana kwa kuripotiwa kwenye vyombo vingi vya Habari.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum nimemnukuu akithibitisha juu ya msiba huo >>> “Ni kweli Mheshimiwa Mufti amefariki.. Kesho saa nne asubuhi Waislamu na Viongozi wote watajumuika Makao Makuu ya BAKWATA, Kinondoni Muslim kuuaga mwili wa Sheikh. Mchana mwili wa Sheikh utasafirishwa kwenda Shinyanga, atazikwa siku ya Alhamisi“>>>– Sheikh Alhadi Mussa Salum
Hapa anamzungumzia Marehemu Mufti Simba>>> “Mufti alikuwa na sifa ya kuwa Kiongozi wa Waislamu. Alikuwa mvumilivu sana na msamehevu katika Utawala wake. Angekuwa hana subira Waislamu wasingekuwa na uvumilivu“>>>– Sheikh Alhadi Mussa Salum
Hapa nina sauti niliyomrekodi Sheikh Alhadi Mussa Salum akizungumzia msiba huo na akimzungumzia Marehemu pia.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.